Kiswahili – Femicide Petition

MSWADA WA OMBI LA KUTENGA TAREHE 6 DISEMBA KAMA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPAMBANA NA MAUAJI YA WANAWAKE KWA AJILI YA JINSIA YAO

 

Siku ya Kimataifa ya Haki za Kibinadamu, Disemba 10, 2021:

Visa vya mauaji wa wanawake kwa ajili ya jinsia yao vimeongezeka maradufu duniani. Cha kusikitisha ni kuwa wanaoeneza kitendo hicho mara nyingi hukwepa hukumu kwa sababu ya vizuizi vya kimila au sheria. Kulingana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa inayosimamia maswala ya mihadarati na uhalifu, takriban wanawake mia moja hupoteza maisha kila siku duniani, mikononi mwa wapendwa au familia, kwa ajili ya jinsia yao (UNODC).

Mwezi Machi, 2021, raia wa Uingereza, Sarah Everard, alikamatwa na polisi kwa kisingizio cha kukikuika sheria, na badala ya kuchukuliwa hatua inavyostahili, alidhulumiwa kimapenzi, akauwawa kisha mwili wake kuchomwa. Marisol Cuadras, raia wa Mexico mwenye umri wa miaka kumi na nane aliuawa kwa kupigwa risasi mnamo Novemba 25, 2021, akishiriki maandamano ya kusuta dhuluma za kijinsia dhidi ya wanawake. Visa hivi mara nyingi hufanyika kisiri lakini pia hutendwa hadharani na wasiowajua waathiriwa wao, au hata mikononi mwa maafisa wa serikali.

Visa hivi pia huripotiwa kazini na katika ulingo wa siasa. Wanawake wenye umri wa juu, wale wanaoishi na ulemavu, au hata wanaokabiliwa na ubaguzi wa rangi, kabila, tabaka na wale waliohamia kwingine, wanakabiliwa na hatari zaidi ya kuuwawa kwa ajili ya jinsia yao.

Cha kusikitisha ni kuwa visa hivi vinaendelea kuongezeka, haswa wakati huu wa janga la Corona, ambapo ukatili nyumbani – chanzo kuu cha mauaji ya wanawake kwa ajili ya jinsia – imekithiri. Takwimu za UNODC zinaashiria kuwa katika mwaka wa 2020, mwanamke au msichana moja aliwuawa kila dakika 11. Idadi ya visa hivi huongezeka kwa kiwango kikubwa unapojumuisha aina nyingine ya mauwaji ya wanawake yasiyo moja kwa moja, kama vile vifo vinavyotokana na uzazi. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa inayosimamia maswala ya jamii, UNFPA, zinaashiria kuwa takriban vifo laki tatu huripotiwa kila dakika mbili kutokana na matatizo ya uzazi.

Tangu mwaka 2019, harakati ya Kampeni ya Siku Kumi na Sita Dhidi ya Dhuluma ya Jinsia, almaarufu, Global 16 Days Campaign, imetenga tarehe 6 Disemba kila mwaka kama kumbukumbu la ‘Mauaji ya Montreal’ mwaka 1989, ambapo mwanaume mmoja aliwaua wanawake kumi na nne kwa ajili ya jinsia yao. Siku hii inalojulikana duniani kote kama ‘Siku ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Wanawake’. Licha ya kisa hiki kufanyika miaka thelathini zilizopita, visa vya mauaji ya wanawake vinaendelea kukithiri kisiri na hadharani.

Tunahimiza jamii yote, mashirika na viongozi kuungana nasi kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuitenga tarehe sita Disemba, kama Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Mauaji ya Wanawake kwa Ajili ya Jinsia. Viongozi wa serikali wanatakiwa kuweka mikakati ya kukabiliana na janga hili, ingawa wengi hawajafaulu licha ya kujitolea. Kutengwa kwa siku hii kutaimarisha vita dhidi ya janga hili kwa:

  • KUPIGA MSASA juhudi za kupambana na janga hili
  • KUWARAI VIONGOZI kuu serikalini kuchukua hatua za kukomesha janga hili
  • KUUNGANISHA juhudi zote za kupambana na janga hili na kuwapa nguvu mpya

Kujumuisha muhuri wako katika mswada huu kitaimarisha azma yetu ya kutaka Shirika la Umoja wa Mataifa na viongozi wa serikali, kuchukua hatua za kuzuia visa vya mauaji ya wanawake na wasichana kwa ajili ya jinsia yao.

Jumuika nasi! Muhuri wako utaokoa maisha.

Fuata @16DaysCampaign katika mtandao wa Facebook, Instagram, na Twitter kwa taarifa zaidi kuhusu juhudi zetu. Tembelea tovuti wetu kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kukomesha janga hili.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

Nishi Shah
Mratibu wa harakati ya Global 16 Days Campaign
Barua pepe: 16days@cwgl.rutgers.edu